NA FRANK
KIBIKI, KILOLO
WANAWAKE
wametakiwa kujiunga kwenye vikundi vya kiuchumi na kufanya kazi kwa bidii ili
waweze kuondokana na ugumu wa maisha unaowakabili.
Kiongozi wa
mbio za Mwenge, Rahel Kassanda alitoa wito huo jana wakati akikabidhi hundi ya
sh milioni moja, kwa kikundi cha wanawake cha Tuinuliwe, kilichopo katika
kijiji cha Masukanzi, wilayani Kilolo.
Kassanda
alisema kikundi hicho ni mfano wa kuigwa na wanawake ambao wamekuwa wakisubiri
kupatiwa fedha na waume zao badala ya wao kushiriki katika uzalishaji.
Alisema ikiwa
kundi la wanawake, litataka kuondokana na ugumu wa maisha, ni lazima kuungana
pamoja kwa kuanzisha vikundi ili iwe rahisi kupatiwa mikopo yenye riba naafuu
na hatimaye kuondokana na umaskini.
Aliwataka
wanawake wa kikundi hicho kutumia fedha za kikundi hicho kwa malengo
yaliyokusudiwa mara wanapokopa ili kutoa naafasi kwa wengine kuendelea
kukopesha.
Akisoma taarifa
ya kikundi hicho, Katibu wa kikundi hicho Jumanne Tembo alisema wanawake
waliojiunga kwenye kikundi hicho wamefanikiwa kuondokana na umaskini.
Alisema tayari
serikali kupitia halmashauri ya wilaya ya Kilolo, iliwapatia mkopo wenye
thamani ya sh milioni 4.4 ambazo wametumia kununulia bajaji ya mizigo, ikiwa ni
mradi wa kikundi.
“Tulianza tikiwa
hatuna kitu, tukaweza kuwekeza sh lakini 240, na sasa tumepata mtaji wa sh
milioni 4.4 fedha ambayo kama tungebweteka nyumbani, tusingeipata,” alisema
Tembo.
Mbali na
masuala ya kiunchumi, wanawake hao wamekuwa wakitumia muda mwingi kujifunza
masuala mbali mbali likiwemo janga la ukimwi.
Mwisho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni