Ndugu
Waandishi wa Habari,
Mkoa
utapokea Mwenge wa Uhuru kutoka Mkoa wa Morogoro tarehe 24 Juni 2014.
Makabidhiano yatafanyika katika kijiji cha Ruaha Mbuyuni kuanzia saa 2.00 hadi
saa 3.00 asubuhi.
Maeneo ambako Mwenge utakimbizwa
Baada
ya kuupokea Mwenge wa Uhuru kutoka Mkoa wa Morogoro Mkuu wa Mkoa wa Iringa
atamkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kilolo ili aanze kuukimbiza katika Wilaya yake.
Ukitoka Wilaya ya Kilolo Mwenge wa Uhuru utakimbizwa Katika Halmashauri ya
Wilaya ya Iringa tarehe 25 Juni, 2014, Manispaa ya Iringa utakimbizwa tarehe 26
Juni, 2014 na Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi utakimbizwa tarehe 27 Juni, 2014
kuanzia saa 2.00 hadi saa 3.00 asubuhi.
Ndugu Waandishi wa Habari,
Baada
ya Mwenge wa Uhuru kukimbizwa katika Mkoa wa Iringa utakabidhiwa kwa Mkoa wa
Njombe tarehe 28 Juni, 2014.
Ndugu Waandishi wa Habari,
Mwenge
wa Uhuru ukiwa katika Mkoa wa Iringa utafanya shughuli za kukagua Miradi ya Maendeleo,
kuweka mawe ya msingi, kufufungua na kuzindua jumla ya Miradi ya Maendeleo 42
yenye thamani ya Tsh. 3,109,958,020/=
Aidha,
Mwenge wa Uhuru utatoa ujumbe katika maeneo yote ambako utakimbizwa. Miradi
ambayo itatembelewa na Mwenge wa Uhuru ni miradi ya Barabara, Miradi ya Elimu,
Miradi ya Afya, Miradi ya Kilimo na ufugaji, Miradi ya Vijana na wanawake na
Miradi ya Hifadhi ya Mazingira.
Ndugu Waandishi wa Habari,
Kila
mwaka Mwenge wa Uhuru hubeba ujumbe maalumu ambao hukusudiwa kuwasilishwa kwa
wananchi kuhusu jambo muhimu linalohusu Taifa katika wakati uliopo. Ujumbe
maalumu wa Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2014 unasema: ‘’katiba ni Sheria kuu ya Nchi’’ wenye kauli Mbiu’ jitokeze kupiga kura
ya maoni tupate katiba mpya. Sambamba na ujumbe maalumu, Mwenge wa Uhuru
kila huwa unatoa elimu na kuhamasisha wananchi kupambana na maadui watatu wa
maendeleo ambao ni Rushwa, Matumizi ya Dawa za Kulevya na ugonjwa wa UKIMWI.
Ndugu Waandishi wa Habari,
Ninapenda
kutumia fursa hii kuviomba vyombo vya habari na ninyi waandishi wa habari
kuwahamasishwa wananchi katika Halmashauri zote za Mkoa wa Iringa kujitokeza
kwa wingi kuulaki Mwenge wa Uhuru katika maeneo yote ambako utapita, kushiriki
katika mikesha ya Mwenge pamoja na kupokea ujumbe wa Mwenge wa Uhuru wa mwaka
huu 2014.
Ndugu Waandishi wa Habari,
Ninawasihi
wananchi kuendelea kudumisha amani na utulivu wakati wote ambapo Mwenge wa
Uhuru utakuwa ukikimbizwa katika Mkoa wetu na hata baada ya kuhitimisha Mbio za
Mwenge katika Mkoa wetu.
Ahsanteni
sana kwa kunisikiliza.
MWENGE WA UHURU OYEEE!
IRINGA OYEEE!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni