Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa- IRINGA
Ajali za barabarani zinaweza
kuepukika iwapo waendesha pikipiki watazingatia sheria na kanuni za usalama
barabarani.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa
wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma alipokuwa akizindua gari la kubeba majeruhi
na kufunga mafunzo ya madereva wa pikipiki Mkoani Iringa yaliyofanyika katika
uwanja wa michezo wa kumbukumbu ya Samora mjini Iringa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma (kushoto) akikata utepe kuzindua gari la wagonjwa |
Dkt. Ishengoma amesema “sote
tunatambua kwamba miaka ya hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la ajali za barabarani
zinazosababisha vifo kwa watu wengi. Ajali hizo zinahusisha pikipiki. Ajali
hizo zinaweza kuepukika endapo waendesha na wapanda pikipiki watazingatia
sheria na kanuni za usalama barabarani”.
Aidha, ametoa wito kwa waendesha pikipiki kuacha tabia ya kuendesha
pikipiki bila kupata mafunzo na kutokuwa na leseni, kuzingatia sheria ya kuvaa
kofia ngumu kwa dereva na abiria na kuacha tabia ya kubeba abiria zaidi ya
mmoja katika pikipiki moja.
Dkt. Christine Ishengoma (Mb.) |
Mkuu wa Mkoa wa Iringa ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinza na Usalama Mkoa wa Iringa amewataka watumiaji
wengine wa barabara kuzingatia sheria za usalama barabarani. Vilevile,
amewataka abiria wa mabasi na magari yote kuzingatia ufungaji wa mikanda kwa
usalama wao. Wakati huohuo amekemea tabia ya abiria kushabikia mwendokasi na
kukataa kujazwa kwenye mabasi zaidi ya idadi inayotakiwa.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni