Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa IRINGA
Wananchi wa Kidamali watanufaika na
ghala la mbolea kwa kupata mbolea na pembejeo za kilimo na ongezeko la kipato
kwa kaya.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa
wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma katika hotuba yake ya uzinguzi wa ghala la
mbolea Kidamali wilayani Iringa iliyosomwa na Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya
Uchumi na sekta za Uzalishaji, Adam Swai.
Dkt. Ishengoma amesema kuwa kupitia
ghalalinalozinguliwa leo wananchi wanatarajia kunufaika na uwepo wa wataalamu
wa kampuni ya Yara watakaotoa ushauri kuhusu kanuni za kilimo bora katika
kipindi chote cha kilimo. Manufaa mengine ameyataja kuwa uwepo wa mbolea
mbalimbali za kupandia, mbolea za kukuzia na uwepo wa pembejeo nyingine za
kilimo kama mbegu bora, dawa za magugu, wadudu na magonjwa kwa kipindi chote
cha kilimo. Faida ndingine ni ongezeko la kipato na kuboresha maisha.
Mkuu wa Mkoa amewataka kulitumia
vizuri ghala hilo kwa kiwango kinachopendekezwa na kitaalamu ili wananchi wengi
waweze kuongeza uzalishaji wa mazao kwa kila ekari jambo litakaloongeza mapato.
Amesema kuwa kufanya hivyo kutaongeza uhakika wa chakula katika kaya, kuongeza
kipato na kupunguza umasikini.
Akiongelea mapinduzi ya kilimo, Dkt.
Ishengoma amesema “ili tuweze kuleta mapinduzi ya kilimo na kuongeza uzalishaji
wa mazao ya chakula na biashara kwa wingi kwa kila ekari inayolimwa ni lazima
tulime kitaalamu. Tunatakiwa tupime na kujua hali ya rutuba katika mashamba
yetu. Maeneo mengi rutuba katika udongo imepungua sana. Kuna upungufu mkubwa wa
viini lishe vya Naitrojeni, Fosforasi, Potassium, Boron, Zinc na Sulfur”.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni