Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa
imepatiwa mashine za kisasa za kupima joto kwa wagonjwa kwa lengo la kuboresha
huduma hospitalini hapo.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Robert Salim (kulia) akimkabidhi Mashine Dkt. Issack Mlay |
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Robert Salim (katikati) akimkabidhi Mashine Dkt. Tatu Mbotoi (kushoto) |
Infrared Thermometer |
Kauli hiyo imetolewa na Mganga Mkuu
wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, Dkt. Robert Salim alipokuwa akikabidhi
mashine za kupima joto (Infrared Thermometer) kwa Dkt. Tatu Mbotoni ambaye ni
Daktari wa Magonjwa ya kawaida ya watu wazima mashine (2) na Dkt. Issack Mlay
ambaye ni Daktari wa watoto mashine (1).
Dkt. Salim amesema kuwa lengo la
kukabidhiwa mashine hizo ni kuifanya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa kuwa ya kisasa
katika utoaji huduma kwa wagonjwa. Amesema kuwa mashine hizo ni nzuri kwa
sababu zinauwezo wa kupima joto pasipo kugusana na mgonjwa. Amesema kuwa
mashine hizo ni muhimu hasa katika kipindi hiki ambapo ugonjwa wa Ebola
umeendelea kuwa tishio barani Afrika.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Iringa
ameshukuru kwa msaada huo na kutoa wito kwa wadau wengine kujitokeza kuisaidia
hospitali hiyo ili iweze kutoa huduma kwa wananchi. Aidha, amewataka
waliokabidhiwa mashine hizo kuzitumia vizuri kwa malengo yaliyokusudiwa.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni