Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Mpango wa usalama wa chakula wa kimataifa
unaolenga kupunguza upotevu wa mazao kutokana na magonjwana kuimarisha usalama
wa chakula.
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu
Tawala Mkoa wa Iringa, Nuhu Mwasumilwe katika hotuba yake ya ufunguzi
iliyosomwa kwa niaba yake na Afisa Kilimo Mkuu katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa,
Grace Macha wakati wa uzinduzi wa Kliniki ya Mimea kituo cha rasilimali cha
Kata ya Ifunda wilayani Iringa.
Grace Macha akisoma hotuba |
Huduma nayo ilitolewa papohapo |
Mwasumilwe amesema kuwa Plantwise ni
mpango wa usalama wa chakula wa kimataifa wenyr lengo la kuzisaidia nchi
washirika kuwapatia wananchi maarifa yanayohitajika ili kupunguza upotevu wa
mazao kutokana na magonjwa na kuimarisha usalama wa chakula kwa kupata usahihi
wa taarifa kuhusiana na afya ya mimea.
Amesema kuwa duniani inakadiliwa kuwa
watu bilioni moja wana upungufu wa chakula kila siku na nusu ya idadi hiyo ni
wakulima wadogo wadogo ambao wanategemea mazao kwa chakula na kipato kwa maisha
ya kila siku.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa amesema kuwa
asilimia 40 ya mazao yanayolimwa duniani kote hupotea kutokana na magonjwa na
wadudu waharibifu. Amesema kuwa kutokana na idadi kubwa ya watu duniani
udhibiti na upotevu wa mazao unahitaji hatua za haraka. Amesema kuwa iwapo
upotevu huo utapunguzwa kwa asilimia moja upo uwezekano wa kulisha watu wengi
zaidi. Amesema kuwa katika kufanikisha hilo wakulima wanahitaji ushauri,
watafiti wanahitaji kutoa taarifa sahihi na watunga sera wanahitaji zana kwa
ajili ya kufanya maamuzi.
Akiongelea malengo ya Mpango huo
ameyataja kuwa ni kuwasaidia wakulima wadogo wadogo kupunguza kiwango cha
upotevu wa mazao kutokana na baa la magonjwa ya mimea na wadudu waharibifu.
Ameongeza malengo mengine kuwa ni kutoa taarifa ya mtawanyiko wa wadudu
waharibifu na magonjwa ya mimea na afya ya mimea kote duniani na kuzifanya
taarifa hizo kupatikana kwa urahisi.
Mpango huu wa Plantwise ulianzishwa
mwaka 2002 ukijulikana kama Kliniki ya Mimea Duniani.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni