Ijumaa, 14 Novemba 2014

MKUU WA MKOA MPYA WA IRINGA APOKELEWA KWA SHANGWE IRINGA



Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza amewataka wafanyakazi wa ofisi yake kufanyan kazi kwa umoja na kujituma zaidi ili kufikia malengo ya Mkoa.

Masenza ametoa kauli hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa alipokuwa akiwasalimia wafanyakazi wa ofisi yake muda mfupi baada ya kukaribishwa katika ofisi yake mpya leo Mkoani Iringa.
 
Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu
Masenza amewaita wafanyakazi hao kuwa ni timu ya ushindi. Amesema “hii ni timu ya ushindi kwa sababu Mkuu wa mkoa na Katibu Tawala Mkoa hatuwezi kufanya kazi wenyewe ila tukiwa pamoja tutashinda”. Amesema “ninahitaji sana ushirikiano wenu kutoka katika sakafu ya moyo wangu”. 

Amewataka wafanyakazi hao kushirikishana masuala mbalimbali ya kazi ili kuweza kubaini ugumu unaoweza kujitokeza na kukwamisha utekelezaji wa baadhi ya majukumu ili ufumbuzi wake uweze kupatikana. 

Mkuu wa mkoa wa Iringa ameelekeza kuwa ushirimkiano huo ni lazima uendane na uwajibikaji kwa wakati. Amesema kuwa kila mfanyakazi ana taalamu yake na kusisitiza kuzitumia taaluma hizo katika kuleta mafanikio na tija katika kazi. Aidha, ametoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa imani aliyoionesha kwake na kumaidi kufanya kazi kwa juhudi na maarifa.

Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu amemhakikishia Mkuu wa mkoa kwa niaba ya wafanyakazi wote kumpatia ushirikiano wa kutosha katika kutekeleza majukumu ya serikali. Ameongeza kuwa yale yote aliyoelekeza Mkuu wa Mkoa atayasimamia ili kuleta ufanisi wa kiutendaji katika mkoa.
 
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza akipokea Ua kutoka kwa Scolastica Mlawi, Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimali Watu.
Akielezea matarajio yake baada ya mapokezi ya Mkuu wa Mkoa mpya, Afisa Wanyamapori katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Faustine Majuto amesema kuwa “kwa kuwa Mkuu wa Mkoa ametoka katika Wilaya inayozalisha sana askari wanyamapori nchini (Ilemela) tunategemea ujio wake utaleta chachu katika kupambana na changamoto za ki-uhifadhi kutokana na uzoefu alionao. Amesema kuwa uzoefu wake utasaidia katika kukuza utalii wa mkoa wa Iringa na Kanda ya kusini kwa ujumla kwa kutumia uwepo wa hifadhi ya Ruaha ambayo ni kubwa kuliko zote Afrika Mashariki na ya pili kwa ukubwa barani Afrika, mapori tengefu, jumuiya za wanyamapori na mazingira asilia. 
 
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa akitokea wilaya ya Ilemela alipokuwa Mkuu wa Wilaya.
=30=

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Habari zinazoendelea hivi sasa

SERIKALI KUWEZESHA VIJANA KUKOPA

Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa Serikali itaendelea kuwawezesha vijana kwa kuwatengenezea mazingira mazuri ya mikopo ili waweze k...