Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Matumizi
ya choo bora na kunawa mikono kwa sabuni ni njia bora ya kupunguza magonjwa ya
kuhara kwa asilimia 32.
Kauli
hiyo imetolewa na mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Iringa Dkt. Leticia Warioba, katika
uzinduzi wa maadhimisho ya choo duniani, siku ya kunawa mikono duniani na wiki
ya usafi wa kimkoa yaliyofanyika katika kijiji cha Ifunda wilayani Iringa.
Dkt.
Warioba amesema “matumizi ya choo bora na kitendo rahisi cha kunawa mikono kwa
sabuni ni moja ya njia bora ya kuokoa maisha ya watoto na jamii nzima kwa
ujumla. Kunawa mikono kabla ya kula na baada ya kutoka msalani/chooni hupunguza
kuenea kwa magonjwa ya kuhara na manufaa yake ni ya muda mrefu kwa afya na
ustawi wa watoto na jamii kwa ujumla”.
Amesema
kuwa takwimu zinaonesha kuwa matumizi ya choo bora hupunguza magonjwa ya kuhara
kwa asilimia 32 na kunawa mikono kwa sabuni hupunguza magonjwa hayo kwa
asilimia 50.
Amesema
kuwa shirika la afya duniani limeainisha kuwa watu wengi duniani wanapata au
kumiliki huduma za simu za mkononi kuliko wanaopata huduma za choo bora. Kati
ya watu bilioni 7 duniani kote, watu bilioni 6 wanamiliki au hupata huduma ya
simu na watu bilioni 4.5 tu ndio wanamiliki au hupata huduma ya choo bora.
Amesema kuwa tafsiri hiyo inamaanisha kuwa watu bilioni 2.5 duniani hasa maeneo
ya vijijini hawana huduma ya vyoo.
Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa, Scolastica Mlawi |
Nae
Afisa afya Mkoa wa Iringa, Khadija Haroun amelitaja lengo la maadhimisho hayo
kuwa ni kuihamasisha jamii kuchukua hatua katika kukabiliana na changamoto za
kukosa huduma za choo bora na unawaji wa mikono kwa sabuni na hatimae kumaliza
kabisa tatizo la huduma hizi muhimu. Ameongeza kuwa maadhimisho hayo yanalenga
kuepusha magonjwa yanayoweza kuambukizwa kupitia kukosa huduma za vyoo na
unawaji wa mikono usio wa kitaalamu.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni