Alhamisi, 19 Februari 2015

MKOA WA IRINGA WAJIVUNIA MAFANIKIO YA KIUCHUMI



Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Mkoa wa Iringa unajivunia mafanikio ya kiuchumi yaliyofikiwa hadi kuongeza pato la Mkoa kufikia shilingi milioni 2,755,924.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza alipokuwa akiwasilisha taarifa ya Mkoa wa Iringa kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayefanya ziara ya kikazi Mkoani Iringa katika Ikulu Ndogo ya Iringa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza

Mhe. Masenza amesema kuwa pato la Mkoa wa Iringa limeongezeka kutoka shilingi milioni 1,702,430 mwaka 2010 hadi kufikia shilingi milioni 2,755,924 mwaka 2013. Amesema kuwa pato la mkazi limeongezeka kutoka shilingi 1,740,947 mwaka 2010 hadi kufikia shilingi 1,990,043 mwaka 2013. Amesme kuwa ongezeko hilo ni sawa na asilimia 14. Amesema kuwa pato hilo la Mkoa linaufanya Mkoa wa Iringa kuwa wa pili kitaifa katika kuwa na pato kubwa la mwananchi.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa amesema kuwa pato la Mkoa huchangiwa na shughuli za kilimo, viwanda, biashara, uvuvi, ufugaji wa samaki, ufugaji wa nyuki na biashara ya mazao ya misitu.
=30=

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Habari zinazoendelea hivi sasa

SERIKALI KUWEZESHA VIJANA KUKOPA

Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa Serikali itaendelea kuwawezesha vijana kwa kuwatengenezea mazingira mazuri ya mikopo ili waweze k...