Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kuboresha huduma za afya katika
hospitali na vituo vya afya ili kutoa huduma bora kwa wananchi.
Kauli
hiyo imetolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo
Pinda baada ya kukagua na kuzindua kituo cha Afya Mlowa kilichopo katika
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.
Mhe.
Pinda amesema “serikali yenu inajitahidi na itaendelea kuboresha huduma za afya
katika hospitali na vituo vya afya ili huhakikisha huduma bora kwa wananchi
wake”. Amesema kuwa ni lengo la serikali huona wananchi wake wanakuwa na afya
bora kutokana na huduma bora za afya.
Akiongelea
magonjwa yanayowaathiri zaidi kina mama, Waziri Mkuu ameyataja kuwa ni saratani
ya mlango wa kizazi, fistula na saratani ya matiti. Ameutaka uongozi wa wilaya
ya Iringa kuwaelimisha wananchi juu ya dalili za magonjwa hayo. Amesema kuwa
magonjwa hayo yanatibika pindi dalili zake zinapogundulika mapema. Amesema kuwa
magonjwa haya yasipotibika mapema huweza kusababisha maambukizi mengine kwa
kina mama na kufanya matibabu yake kuwa magumu zaidi na hatimae kusababisha
vifo vinavyoweza kuzuilika.
Kwa
upande wa magonjwa yanayowakabili wanaume kwa wingi, ameyataja kuwa ni
shinikizo la damu na saratani ya tezi dume. Amesema wanaume wengi wanakabiliwa
na shinikizo la damu kutokana na wingi wa majukumu waliyo nayo.
Katika
taarifa ya mradi wa ujenzi wa kituo cha afya Mlowa iliyosomwa kwa Waziri Mkuu
na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Bibi Pudenciana Kisaka
amesema kuwa kutokana na umuhimu wa sekta ya afya katika halmashauri ya wilaya
ya Iringa, iliamua kuchangia shilingi 61,534,000. Amesema kuwa wadau wengine waliochangia
ni serikali ya Japan kupitia Jica iliyochangia shilingi 111,000,000 na wadau
wengine wa maendeleo hadi kufikia shilingi 197,789,000.
Kituo
cha afya Mlowa kinahudumia wananchi 4,347 wa vijiji vya Malinzanga, Mafuruto na
Nyamahana.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni