Jumanne, 17 Februari 2015

WAZIRI MKUU KUZURU MKOA WA IRINGA


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda (Mb.) anaanza ziara ya kikazi Mkoani Iringa leo. Katika ziara hiyo inayoanza tarehe 18-22 Februari, 2015 itahusisha kutembelea Wilaya zote tatu za Mkoa wa Iringa. Wilaya hizo ni Iringa, Kilolo na Mufindi. 
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda
WaziriMkuu anatarajiwa kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Iringa majira ya saa 9 alasiri na kupokelewa na viongozi wa Mkoa wa Iringa. 

Ziara yake ya kwanza itaanzia katika Chuo kikuu cha Mkwawa ambapo atakagua Maendeleo ya Mradi wa STHEP.

Saa 11:30 Jioni Waziri Mkuu atasomewa Taarifaya Maendeleo ya Mkoa wa Iringa  na Wilaya ya Iringa katika uwanja wa Ikulu Ndogo mjini Iringa.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Habari zinazoendelea hivi sasa

SERIKALI KUWEZESHA VIJANA KUKOPA

Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa Serikali itaendelea kuwawezesha vijana kwa kuwatengenezea mazingira mazuri ya mikopo ili waweze k...