Jumapili, 1 Machi 2015

PINDA AWATAKA WANANCHI KUJIUNGA SACCOS



Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda amewataka wananchi wengi kujiunga na SACCOS nchini ili ziweze kuwakomboa.
Kauli hiyo ameitoka katika ziara yake ya kukagua SACCOS ya Mazombe iliyopo wilayani Kilolo mkoani Iringa.
“Nawahimiza wananchi wengi wajiunge na SACCOs hizi. Aidha, viongozi wa SACCOs msiogope kukopa benki. Nitaongea na Bwana Kimei wa benki ya CRDB tuone uwezekano wa kuipatia SACCOs ya Mazombe mkopo” alisema Mhe. Pinda.
Waziri Mkuu amewataka viongozi wa SACCOS kusimamia taarifa za mapato na matumzi mara kwa mara kwa mujibu wa sheria na taratibu na kanuni za SACCOS zenyewe.
Waziri Mkuu amefurahishwa na juhudi zilizooneshwa na wananchama wa Mazombe SACCOS. Amesema mafanikio yao yanadhihirisha kuwa SACCOS hiyo ni mkombozi wa wanyonge.
SACCOS ya Mazombe ina mtaji wa shilingi Milioni 859 ikiwa imekopesha mikopo ya shilingi Bilioni 4.
=30=

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Habari zinazoendelea hivi sasa

SERIKALI KUWEZESHA VIJANA KUKOPA

Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa Serikali itaendelea kuwawezesha vijana kwa kuwatengenezea mazingira mazuri ya mikopo ili waweze k...