Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Vijiji zaidi ya 20 vimesambaziwa huduma ya umeme
na REA Mkoani Iringa kufikia mwaka 2014.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa
Iringa, Mhe. Amina Masenza katika taarifa aliyoisoma kwa Waziri Mkuu wa
Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda Ikulu ya Iringa.
Mhe. Masenza amesema kuwa Wakala wa Umeme Vijijini
(REA) wamefanikiwa kusambaza umeme katika vijiji mbalimbali vya Mkoa wa Iringa.
Katika kipindi cha mwaka 2010-2014 jumla ya vijiji 21 vilikuwa vimepewa huduma
ya umeme. Amesema kuwa kwa mwaka wa fedha 2014/2015, REA wanatarajia kuvipatia
huduma ya umeme vijiji 94 katika Mkoa wa Iringa.
Akiongelea miradi ya umeme vijijini katika
majumuisho ya ziara yake Mkoani Iringa, Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda
ameitaka Wizara ya Nishati na Madini na Wakala wa Umeme Vijijini kuongeza kasi
ya usambazaji ili vijiji vingine viweze kupata umeme mapema iwezekanavyo.
Amesema kwa mujibu wa mtandao wa Wakala wa
Umeme Vijijini, vijiji vitakavyopatiwa umeme kwa Mkoa wa Iringa kwa Grid ya Taifa
2014/2015 kuwa ni vijiji vya Idodi, Tungamalenga, Hifadhi ya
Taifa Ruaha, Pawaga, Ikuvilo, Isimila, Mlanda, Ng’enza, Mgama, Kiponzero,
Itengwilinyi, Lupembe, Lwasenga, Kiwere, Mfihome, Muhefu na Kitapilimwa (Vijiji
17) vyote Iringa vijijini.
Vingine ni vijiji vya Ilamba, Lukani,
Ihimbo, Utengule, Ibumi, Image, Mtitu, Pomerine, Bomalang’ombe, Mwatasi, Stendi
ya Mbuzi, Imalutwa, Lugalo, Kitumbuka, Luganga-Kibaoni, Lusinga, Shule ya
Sekondari Udzungwa, Dabaga, Irole na Maria Consolata (Vijiji 20) katika Wilaya
ya Kilolo.
Vijiji vingine ni Kibengu, Usokami, Mapanda,
Ukami, Ihimbo, Ilongombe, Kipanga, Igeleke, Uhafiwa, Ihalamba, Wamia, Vikula,
Nundwa, Ugesa, Kidilu, Ilusa, Madibira, Idofi, Nyigo, Iramba, Mbalamaziwa,
Malangali Sekondari, Ihowanza, Kwatanga, Ikongozi, Kilimanzowo, Mtambula,
Udumuka, Lugolofu, Ihomasa na Kituo cha Afya Nyololo (Vijiji 32) katika Wilaya
ya Mufindi.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni