Ijumaa, 17 Julai 2015

MKUU WA MKOA AWATAKIA IDDI NJEMA WANANCHI WA IRINGA



Mkuu wa mkoa wa Iringa, Mheshimiwa Amina Masenza amewatakia heri ya sikukuu ya Iddi wananchi wote na kuwataka kusherehekea katika hali ya amani na utulivu.
 





Mheshimiwa Masenza ameyasema hayo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari wa mkoa wa Iringa jana ofisini kwake.
Mheshimiwa Masenza amewapongeza waislamu wote kwa mfungo mtukufu wa Ramadhan na kuwatakia heri katika sikukuu ya Iddi yenye baraka tele.

Amewahakikishia kusherehekea vizuri na kusema kuwa vyombo vya usalama vipo macho muda wote kuhakikisha amani na usalama vinakuwepo wakati wote.
Kufuatia fununu za kusudio la kufunga maduka mjini Iringa, mkuu wa mkoa amewahakikishia wananchi wa mkoa wa Iringa kuwa maduka hayatafungwa na wananchi wanedelee na ratiba zao za kununua mahitaji kadri watakavyojaaliwa. Amesema kuwa ameongea na Mwenyekiti wa wafanyabiashara na kumtaka kutokufunga maduka hayo. Ameongeza kuwa iwapo kuna tatizo wakutane mezani baada ya mapumziko ya sikukuu na kujadili kwa pamoja.
=30=

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Habari zinazoendelea hivi sasa

SERIKALI KUWEZESHA VIJANA KUKOPA

Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa Serikali itaendelea kuwawezesha vijana kwa kuwatengenezea mazingira mazuri ya mikopo ili waweze k...