Na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Ofisi
ya mkuu wa mkoa wa Iringa imekabidhi zawadi za sherehe ya Eid El Fitri kwa
makao ya watoto ya Dar-bilaal & Dar-fatma.
Zawadi
hizo zilikabidhiwa na mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza katika makao ya
watoto yaliyopo eneo la Ilala mjini Iringa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza akikabidhi zawadi za Eid El Fitri |
Masenza
alisema kuwa ofisi yake inatambua kuwa jukumu la malezi ya watoto walio katika
mazingira magumu si jukumu la taasisi ya Dhi Nureyn pekee bali jukumu la jamii
nzima. Aidha, alitoa rai kwa jamii nzima kuwasaidia watoto wanaolelewa katika
makao ya watoto yaliyopo mkoani Iringa.
Zawadi
zilizotolewa na Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa ni mchele kilo 150, mbuzi
mmoja, sabuni katoni tano na mifuko mitano ya peremende.
Mkuu
wa makao hayo ya watoto Ally Hassan alishukuru kutembelewa na mkuu wa mkoa na
katibu tawala mkoa na zawadi walizopatiwa. Alisema kuwa kutokana na zawadi hizo
watoto hao watasherehekea vizuri sikukuu ya Eid el Fitri.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni