Na. Mwandishi Maalum, Iringa
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji nchini ameombwa kuangalia uwezekano wa
kubadilisha tenki la maji kutoka katika magari ya Zimamoto ambayo hayafanyi
kazi ili lihamishiwe katika gari lililopata ajali mkoani Iringa kuendelea kutoa
huduma.
Ombi hilo
lilitolewa na mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza alipokuwa akishukuru baada
ya kukabidhiwa msaada wa gari la Zimamoto na uokoaji kutoka kwa mdau wa
maendeleo katika mkoa wa Iringa, Zacharia HansPope katika kituo cha Zimamoto na
uokoaji mjini Iringa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza (kushoto) na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye (kulia) wakiteta jambo |
Masenza alisema
“kwa kuwa gari lililopata ajali
limeharibika tenki la kuhifadhia maji, nikuombe uangalie uwezekano wa kuhamisha
tenki kwenye magari yako yaliyopaki ili lije kufanya kazi mkoani Iringa”.
Alisema kuwa upatikanaji wa tenki hilo utasaidia gari lililopata ajali kuanza
kufanya kazi tena kwa gharama nafuu zaidi.
Mkuu wa mkoa
aliwataka wakazi wa Iringa kuiga mfano nzuri wa Zacharia HansPope wa utayari wa
kuchangia shughuli za maendeleo kwa mkoa wa Iringa.
Wakati huohuo
Mkuu wa Mkoa wa Iringa alipongeza utendaji kazi wa Kamanda wa Zimamoto mkoa wa
Iringa, Mrakibu kennedy Komba. “Kamanda wa
Jeshi la Zimamoto na uokoaji Mkoa wa Iringa ni mtu makini katika utendaji wake,
amekuwa akinipa ushirikiano sana, pia yupo haraka katika utoaji wa Taarifa na
kuchukua hatua sahihi” alisema mkuu wa Mkoa.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni