Halmashauri
ya wilaya ya Kilolo imejipanga kuongeza ushiriki wa vijana katika shughuli za
kilimo na ufugaji ili kuwahakikishia ajira ya kudumu.
Kauli
hiyo ilitolewa na mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kilolo, Vallence
Kihwaga alipokuwa akijibu maswali ya wanahabari baada ya kutembelea banda la Halmashauri
ya wilaya ya Kilolo jana.
Kihwaga
alisema “Halmashauri ya wilaya ya Kilolo
inaendelea kutekeleza mpango wa kuwavutia vijana ili wajiingize katika shughuli
za kilimo na ufugaji. Vijana wengi wamekuwa wakizipa kisogo shughuli za kilimo
na ufugaji, hivyo Halmashauri yangu inaendelea kuwavutia vijana wengi
kujiingiza katika kilimo”. Aliongeza kuwa Halmashauri yake imetenga maeneo
kwa ajili ya shughuli za vijana.
Mwenyekiti
huyo alisema kuwa katika maonesho ya Nanenane mwaka 2018 Halmashauri yake
itapeleka wakulima wa kutosha kutoka kila Kata kujifunza ili wakawe chachu ya
mabadiliko ya sekta ya kilimo na mifugo wilayani Kilolo.
“Msimu huu, Halmashauri tumeamua kuleta waheshimiwa Madiwani wote wa
Halmashauri ili wanaporudi wakawe injini ya kusukuma shughuli za kilimo na
mifugo kwa wananchi wanaowasimamia” alisema Kihwaga.
Maonesho
ya shughuli za wakalima Nanenane mwaka 2017 yanaongozwa na kaulimbiu isemayo, “zalisha
kwa tija mazao na bidhaa za kilimo, mifugo na uvuvi kufikia uchumi wa kati”.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni