Na. Dennis Gondwe, Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa wa Iringa
Halmashauri
ya mji wa Mafinga imetumia maonesho ya Nanenane kujifunza fursa zinazoweza
kuwanufaisha wananchi wa Mafinga.
Kauli
hiyo ilitolewa na mkurugenzi wa mji wa Mafinga, Saada Mwaruka alipokuwa
akielelezea umuhimu wa Halmashauri yake kushiriki katika maonesho ya Nanenane
mjini Mbeya jana.
Mwaruka
alisema “ushiriki wa Halmashauri ya mji
wa Mafinga katika maonesho ya Nanenane ni fursa ya kubaini na kujifunza fursa
mbalimbali za kilimo, mifugo na uvuvi ambazo zitaweza kuwanufaisha wananchi
wetu”.
Akiongelea
fursa za kilimo zilizopo katika Halmashauri ya mji Mafinga, mkurugenzi huyo
alisema kuwa Halmashauri yake inayo maeneo mazuri yanayofaa kwa ajili ya kilimo
cha mazao mbalimbali ya chakula na bustani.
Aliyataja mazao yanayolimwa kuwa ni
mahindi, alizeti na maharage. Fursa nyingine alizitaja kuwa ni ufugaji wa
ng’ombe, kuku na mifugo mingine.
Mwaruka
alisema kuwa Halmashauri yake yenye hekta zaidi ya 64,000 zinazofaa kwa kilimo
imejipanga kuongeza uzalishaji na tija ili kufikia uchumi wa kati.
Maonesho ya shughuli za wakalima Nanenane
mwaka 2017 yanaongozwa na kaulimbiu isemayo, “zalisha kwa tija mazao na bidhaa
za kilimo, mifugo na uvuvi kufikia uchumi wa kati”.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni