Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Kamati
ya ulinzi na usalama mkoa wa Iringa kuongoza operesheni ya kuwaondoa wakulima
katika bonde la Nyaluu katika kudhibiti ujangili katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha.
Kauli
hiyo ilitolewa na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Iringa,
Amina Masenza katika kuhitimisha ziara ya waziri wa maliasili na utalii
wilayani Iringa jana.
Masenza
ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Iringa alisema kuwa shughuli zote za kibinadamu
ndani ya eneo la Nyaluu haziruhusiwi na eneo hilo lihifadhiwe. Aidha, alishauri
kambi ya doria ijengwe katika eneo hilo ili kurahisisha udhibiti wa ujangili
katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha na eneo hilo ambalo ni mapito ya wanyama na
eneo la jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori Pawaga na Idodi (Mbomipa) kwa ujumla.
Aidha, aliitaka halmashauri ya wilaya ya Iringa kuorodhesha wakulima wote wanaolima katika bonde la Nyaluu na kuwaandikia barua ya zuio la kulima eneo hilo.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni