Na. Dennis Gondwe, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa
Wakulima
na wajasiriamali watakiwa kuweka utaratibu wa kutunza kumbukumbu za mahesabu
ili kubaini faida na hasara inayopatikana katika shughuli zao.
Kauli
hiyo ilitolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu alipokuwa akifanya
majumuisho ya ziara ya kukagua mabanda alipomuwakilisha mkuu wa mkoa wa Iringa,
Amina Masenza.
Ayubu
alisema “ni vizuri wakulima na wajasiriamali wakafundishwa jinsi ya kutunza
kumbukumbu za mahesabu ya kilimo na uzalishaji ili kufahamu gharama na mwenendo
mzima wa kazi wanazofanya. Kufanya hivyo kutamsaidia mkulima na mjasiriamali
kujua hali halisi ya kazi anayofanya na kuwawezesha kutoa ushuhuda”.
Katibu
Tawala Mkoa wa Iringa aliwataka wakurugenzi kuhakikisha wanawapangia malengo
maafisa ugani ili waweze kutoa tija katika shughuli za kilimo na mifugo.
“Hakikisheni wataalam hawa mnawapangia
malengo yanayopimika na wawe na mpango kazi unaotekelezeka. Utaratibu huu
utawawezesha wakulima na wafugaji kuhudumiwa” alisisitiza Ayubu.
Akiongelea
uzalishaji katika mashamba ya kuzalisha mitamba ya serikali ya Kitulo na Sao-Hill,
Katibu Tawala Mkoa aliyatka mashamba hayo kuongeza uzalishaji wa mitamba ili
kukidhi mahitaji ya mitamba katika mikoa ya nyanda za kuu kusini.
“Mahitaji ya mitamba ni makubwa kwa mikoa ya
nyanda za juu kusini, hivyo soko ni la uhakika. Kinachotakiwa ni kuzalisha
mitamba zaidi” alisisitiza Ayubu.
Aidha, aliyakata mashamba hayo kuongeza
matumizi ya teknolojia katika uzalishaja wa mitamba.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni