Jumatatu, 7 Agosti 2017

MOBISOL KUPELEKA HUDUMA VIJIJINI



Na. Dennis Gondwe, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa

Kampuni ya inayohusika na bidhaa za umeme wa jua (Mobisol) imetakiwa kupeleka huduma zake vijijini ambapo hakuna huduma za umeme ili kuwanufaisha wananchi wengi.

Kauli hiyo ilitolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu alipotembelea banda ya Mobisol katika uwanja wa maonesho ya Nanenane wa John Mwakangale mjini Mbeya. 

Ayubu alisema kuwa kampuni hiyo inafanya kazi nzuri ya kuhakikisha huduma ya umeme wa jua unawafikia wananchi wengi zaidi. 

Mobisel mnafanya kazi nzuri, mnatakiwa kujikita pia vijijini ili wananchi wengi wanufaike na huduma ya umeme wa jua kwa sababu baadhi ya maeneo hayana huduma ya nishati ya umeme" alisisitiza Ayubu. 

Aidha, aliwataka kuendeleza huduma ya ufundi kwa vijana wengi ili kutengeneza mitambo ya umeme wa jua pindi inapoharibika. 
=30=

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Habari zinazoendelea hivi sasa

SERIKALI KUWEZESHA VIJANA KUKOPA

Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa Serikali itaendelea kuwawezesha vijana kwa kuwatengenezea mazingira mazuri ya mikopo ili waweze k...