Na Mwandishi Maalum, IRINGA
Mkoa
wa Iringa ni kitovu kikuu cha kuendelea utalii kwa mikoa ya nyanda za juu
kusini kwa mujibu wa mipango ya wizara ya Maliasili na Utalii ya kuendeleza
utalii nchini.
Kauli
hiyo ilitolewa na waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe wakati
wa kufungua maadhimisho ya siku ya utalii Duniani, maonesho ya Karibu Kusini na
maonesho ya shughuli za viwanda vidogo (SIDO) mjini Iringa jana.
Prof.
Maghembe alisema “napenda kuchukua fursa
hii kuendelea kuwakumbusha mipango yetu juu ya maendeleo ya utalii ukanda wa
kusini. Kwa mujibu wa mpango kabambe wa kuendeleza utalii nchini wa mwaka 2002
(integrated Tourism Master Plan 2002), Iringa ni kituo kikuu (hub) ya maendeleo
ya utalii ukanda wa kusini”.
Aliongeza kuwa tayari juhudi za kufanikisha jambo
hilovzinaendelea vizuri. “Kupitia mradi
resilient natural resources management for growth, pamoja na mambo mengine
tunalenga kuimarisha miundombinu ya ndani ya hifadhi, kuboresha vivutio vya
utalii, kuhamasisha uwekezaji wa biashara za utalii kuimarisha utangazaji,
kujenga ofisi ya wizara ya kanda” alisema Prof. Maghembe.
Nae
mkuu wa mkoa wa Iringa, mheshimiwa Amina Masenza alisema kuwa mkoa wake daima
utakuwa mstari wa mbele kuhakikisha sekta ya utalii inakuwa ya mfano na kukua
kwa kasi.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni