Na Mwandishi Maalum, IRINGA
Mkoa
wa Iringa uliteuliwa kuwa kitovu cha utalii kwa mikoa ya nyanda za juu kusini
kwa maana ya kuwa kichocheo cha kukuza uchumi kwa ukanda wa kusini.
Kauli
hiyo ilitolewa na mkuu wa mkoa wa Iringa, mheshimiwa Amina Masenza katika
salamu zake katika ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya utalii Duniani, maonesho
ya Karibu Kusini na shughuli za viwanda vidogo (SIDO), yaliyofanyika katika
uwanja wa kichangani Manispaa ya Iringa jana.
Mheshimiwa Masenza
alisema kuwa mkoa wa Iringa uliteuliwa kuwa kitovu cha utalii kwa mikoa ya
kusini na wizara ya Maliasili na Utalii mwaka 2002. Alisema katika mwaka huo
maonesho ya Utalii Karibu Kusini yalifanyika kwa mara ya kwanza katika ukanda
huo.
“Kwa msingi huo tupo hapa leo
kuendeleza jitihada hizo za kuendeleza utalii. Lakini kwa kuwa serikali yetu
inahimiza maendeleo ya viwanda, maonesho haya ya Utalii ya Karibu Kusini
yanafanyika sambamba na maonesho ya shughuli za wajasiriamali (SIDO) katika
kuenzi na kuendeleza maendeleo ya viwanda” alisema Masenza.
Mkuu
wa mkoa wa Iringa, alisema kuwa hulka ya sekta ya utalii, maendeleo yake
yanategemea na sekta nyingine, “mikoa ya
nyanda za juu kusini inatupasa kuendeleza sekta nyingine kama kilimo, ufugaji,
usindikaji wa bidhaa mbalimbali, matumizi ya teknolojia bora na nafuu,
uanzishwaji wa miradi mbalimbali ya utunzaji mazingira na kutafuta mitaji na
masoko kwa ajili ya kukuza biashara ya utalii” alisema Masenza.
Aidha,
aliahidi kuwa mkoa wake daima utakuwa mstari wa mbele kuhakikisha sekta ya
utalii inakuwa ya mfano na kukua kwa kasi.
Siku
ya utalii Duniani, maonesho ya Utalii Karibu Kusini na shughuli za viwanda
vidogo SIDO yanalenga kuelimisha umuhimu wa sekta ya utalii na viwanda kwa
maendeleo ya wananchi wa mikoa ya kusini.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni