Na Mwandishi Maalum, IRINGA
Maonesho
ya utalii karibu kusini na wajasiriamali wa SIDO yatumike kutangaza shughuli,
fursa na vivutio vilivyopo mikoa ya nyanda za juu kusini.
Kauli
hiyo ilitolewa na waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe wakati
wa kufungua maadhimisho ya siku ya utalii Duniani, maonesho ya Karibu Kusini na
maonesho ya shughuli za viwanda vidogo (SIDO) mjini Iringa jana.
Prof
Maghembe alisema “kipekee nimefurahishwa na maonesho ya karibu kusini mwak 2017
ambayo kwa mwaka huu yamejumuisha wajasiriamali wa SIDO ambao ni wazalishajai
wa bidhaa mbalimbali zinazoweza pia kutumiwa na watalii na kutoa huduma za
kitalii nchini. Karibu kusini ni fursa ya kutangaza vivutio vya utalii
vilivyopo katika mikoa ya nyanda za juu kusini na kuhamasisha wananchi na wadau
mbalimbali kutembelea vivutio hivyo”. Aliongeza kuwa nchi ya Tanzania ina
maeneo mengi yenye fursa za uwekezaji ambazo hazijaendelezwa ipasavyo.
Aliyataja
maeneo hayo kuwa ni ukanda wa nyanda za juu kusini wenye vitutio vingi na
vizuri vya utalii wakiwemo wanyama pori. Vivutio vingine alivitaja kuwa ni
hifadhi za misitu asili, mandhari nzuri za kuvutia, bonde la Usangu na mto
Ruaha, ziwa Nyasa na Kimondo. “Vivutio
hivi hutoa fursa na kuendeleza utalii katika ukanda huu. Aidha, ni wakati
muafaka wa kuzitangaza fursa hizi ili kuvutia wawekezaji waje kuwekeza katika
ukanda huu” alisema Prof. Maghembe.
Nae
mkuu wa mkoa wa Iringa, mheshimiwa Amina Masenza alisema kuwa mkoa wake daima
utakuwa mstari wa mbele kuhakikisha sekta ya utalii inakuwa ya mfano na kukua
kwa kasi.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni