Jumapili, 1 Oktoba 2017

MIKOA YA NYANDA ZA JUU KUSINI KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII



Na Mwandishi Maalum, IRINGA
Mikoa ya nyanza za juu kusini imetakiwa kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo katika mikoa yao ili vifahamike na kutoa fursa ya kukuza uchumi wa wananchi.

Kauli hiyo ilitolewa na naibu waziri wa maliasili na utalii mhandisi Ramo Makani katika salamu zake katika ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya utalii Duniani, maonesho ya Karibu Kusini na shughuli za viwanda vidogo (SIDO), yaliyofanyika katika uwanja wa kichangani Manispaa ya Iringa jana.
 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng Ramo Makani (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Jamhuri William (kulia. Nyuma ni Katibu Tawala Mkoa wa Iringa
Mhandisi Makani alisema kuwa mikoa ya nyanda za juu kusini ina vivutio vingi na vya kipekee. Alisema kuwa vivutio hivyo vikitangazwa na kufahamika kwa watu watavutiwa kuvitembelea na kununua bidhaa zinazotokana na utalii.

Aidha, aliitaka sekta binafsi kushiriki kikamilifu katika kukuza utalii kwa kanda ya nyanda za juu kusini. Alisema kuwa sekta binafsi ina mchango muhimu sana katika kukuza uchumi.
=30=

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Habari zinazoendelea hivi sasa

SERIKALI KUWEZESHA VIJANA KUKOPA

Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa Serikali itaendelea kuwawezesha vijana kwa kuwatengenezea mazingira mazuri ya mikopo ili waweze k...