Na Mwandishi Maalum, IRINGA
Wakala
wa barabara nchini (TANROADS) mkoa wa Iringa kuendelea kujenga na kuimarisha
barabara ili watalii waweze kunufaika na huduma ya usafiri bora.
Kauli
hiyo ilitolewa na msimamizi wa banda la TANROADS mkoa wa Iringa, Subira
Anyisile alipokuwa akielezea nafasi ya TANROADS katika kukuza sekta ya utalii
mkoa wa Iringa kwenye siku ya utalii duniani, maonesho ya utalii karibu kusini
na shughuli za wajasiriamali wa viwanda vidogo - SIDO katika uwanja wa
Kichangani mjini Iringa.
Anyisile alisema kuwa Wakala wa barabara una mchango mkubwa katika kukuza sekta ya
utalii nchini.
“Sisi TANROADS tunahusika
na ujenzi na ukarabati wa barabara nchini. Utakubaliana nami kuwa barabara
ndiyo kichocheo kikubwa cha kukuza sekta ya utalii nchini. Watalii hawawezi
kufika mbugani au katika eneo la kivutio cha utalii bila barabara” alisema
Anyisile.
Katika kuhakikisha watalii wa ndani na nje wanaendelea kufurahia
huduma za barabara, TANROADS imekuwa ikifanya ukarabati mkubwa na mdogo katika
baadhi ya barabara zake ili zipitike muda wote. Alisema kuwa lengo la ujenzi na
ukarabani wa barabara ni kurahisisha usafiri na kuchochea watalii kutembelea
maeneo ya vivutio na kuuza na kununua bidhaa za kitalii.
“Katika biashara hiyo
mzunguko wa fedha unakuwepo na uchumi unakuwa kwa sababau maeneo mengi yanafunguka
baada ya kuwa na mtandao wa barabara” alisema Anyisile.
Akiongelea
ujenzi wa barabara inayoelekea hifadhi ya Taifa ya Ruaha (Iringa- Msembe) kwa
kiwango cha lami, Anyisile alisema kuwa upembuzi na usanifu umekamilika
zinasubiriwa fedha tu.
Wakala
wa barabara mkoa wa Iringa unasimamia mtandao wa barabara wenye urefu wa km
1,192.9, kati ya hizo km 417.1 ni za lami na km 775.8 ni changarawe.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni