1.0
UTANGULIZI
Ndugu. Mgeni
rasmi,
Katibu Tawala wa Mkoa. Mkoa wa Iringa unaadhimisha wiki ya maji kwa mara
ya 26, tangu maadhimisho haya yalipoanza kuadhimishwa hapa nchi kwa mara ya
kwanza mwaka 1988. Maadhimisho haya yaliongezwa nguvu na umuhimu na Azimio Na. 47/193
la 22 Desemba, 1992 la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Wiki ya maji huunganisha wadau wa
Sekta mbalimbali katika kutathimini na kupanga jinsi ya kuboresha upatikanaji
na utumiaji wa rasilimali za maji kwa manufaa ya wote. Mkoa wa Iringa unaungana
na Watanzania wote katika maadhisho ya wiki ya maji ya mwaka huu yenye kaulimbiu
isemayo ‘Uhakika wa Upatikanaji Maji na
Nishati’
Nanukuu
‘By the resolution 47/193 of 22 December 1992, the
General Assembly declared 22 March of each year World Day to remind everybody
that concrete efforts to provide clean drinking water and increase awareness
world-wide of the problems and of the solutions, can help make the difference. DO YOUR PART. PLEASE USE WATER WITH CARE.
REMEMBER THOSE PLACES WITH NO WATER OR POOR WATER QUALITY’.
Ndugu Mgeni Rasmi
Maadhimisho
haya ni ya 26 na hufanyika kila mwaka kuanzia tarehe 16 hadi 22 mwezi
Machi. Maadhimisho ya mwaka huu yanafanyika Kitaifa Mjini Dodoma. Aidha,
Kimkoa yanafanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo na hususan
yanazinduliwa katika kijiji cha Ihimbo.
Ndugu Mgeni Rasmi.
Kaulimbiu ya
wiki ya maji ya mwaka huu inatukumbusha jinsi ambavyo uhusiano wa upatikanaji
wa huduma ya maji unavyotegemeana na upatikanaji wa huduma ya nishati, hususan
nishati ya umeme (hydro power). Hivyo, kuboresha kitu kimoja ni kuboresha vitu
vyote viwili.
2.0
HUDUMA YA MAJISAFI
2.1
Maji Mijini
Wananchi wanaopata huduma ya majisafi Mijini
katika Mkoa wa Iringa 189,644 kati ya wananchi 247,156 ambao ni sawa na
asilimia 76.7 ya wanchi waishio mijini. Hali ya huduma ya maji Mijini
inategemewa kuongezeka mara baada ya kutekelezwa kwa miradi katika miji ya
Ilula, Kilolo na Mafinga. Miradi hii inategemewa kutekelezwa kupitia program ya
Maendeleo ya Sekta ya Maji (WSDP) ambapo jumla ya wananchi 57,512 watapata
huduma bora ya majisafi na salama.
3.0 Hali ya Upatikanaji wa Huduma ya Maji Vijijini
Jumla ya wananchi wapatao
441,170 sawa na 63.6 % ya wananchi wote waishio vijijini wanapata huduma ya
maji safi na salama kupitia miradi iliyojengwa kwa kutumia teknolojia
mbalimbali zikiwemo:- visima virefu na vifupi, maji ya bomba na visima vya
asili na chemichemi zilizo boreshwa. Upatikanaji wa huduma ya maji kwa upande
wa vijijini kwa kila wilaya ni kama ifuatavyo: -
i)
Halmashauri ya
Manispaa ya Iringa (vijijini - peri urban) inatoa huduma ya maji kwa wananchi
wapatao 8,668, sawa na asilimia 76.2
ii)
Halmashauri ya
Wilaya ya Iringa inatoa huduma ya maji kwa wananchi wapatao 172,742, sawa na
asilimia 68.0
iii)
Halmashauri ya
Wilaya ya Kilolo inatoa huduma ya maji kwa wananchi wapatao 94,288, sawa na
asilimia 57.9
iv)
Halmashauri ya
Wilaya ya Mufindi inatoa huduma ya maji kwa wananchi wapatao 159,763, sawa na
asilimia 60.1
Utoaji wa
huduma unatarajia kuongezeka mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa miradi ya maji
katika vijiji kumi kwa kila Halmashauri.
4.0 Ujenzi wa miradi ya matokeo makubwa sasa (BRN)
Ndugu Mgeni Rasmi.
Mkoa unajenga
miradi 42 ya maji yenye kuleta matokeo makubwa sasa. Miradi hiyo iko katika
hatua mbalimbali ya ujenzi, aidha mkoa unahitaji kiasi cha Tshs. Bilioni 11.582
kwa ajili ya kuwalipa Makandarasi, Wataalam Waelekezi na usimamizi na
ufuatiliaji wa ujenzi wa miradi hiyo.
5.0 Wadau
wa Maji
Ndugu
Mgeni rasmi.
Mkoa unasharikiana vizuri na wadau
mbalimbali katika ujenzi na utoaji wa huduma ya maji na usafi wa mazingira,
wadau hao ni pamoja na Living Water International, Rural Development Organization,
Kanisa la RC, St. Paul Partners, MLFM and AVSI, IDYDC kupitia program ya MAUWA,
Emmanuel International na UNICEF
6.0 Mifuko
ya maji
Ili
kuwa na miradi endelevu uundaji wa kamati za maji na vyombo imara vya
watumiamaji ni jambo la msingi. Kwa mantiki hiyo Mkoa una jumla ya kamati za
maji ni 162, mifuko ya maji 143 na vyombo vya watumia maji 10.
7.0 Hali
ya Watumishi wa Kada za Maji
Mkoa
una jumla ya watumishi 64 wa kada za maji, wakiwemo Wahandisi, Mafundi sanifu
na Mafundi sanifu wasaidizi. Kwa ujumla Mkoa unaupungufu wa wataalam wa kada za
maji 31.
Ndugu Mgeni Rasmi
8.0 Changamoto Mbalimbali Zinazoikabili Sekta ya Maji Huduma ya Maji na usafi wa Mazingira
i.
Wananchi
kutochangia kikamilifu mifuko ya maji vijijini kutokana na uelewa mdogo wa sera
ya maji ya mwaka 2002.
ii.
Wananchi
kutotunza miradi ya maji mara baada ya miradi kukamilika na kukabidhiwa kwa
wananchi
iii.
Wananchi
kuharibu vyanzo vya maji kwa kufanya shughuli za kibinadamu ndani ya maeneo ya
vyanzo vya maji.
iv.
Uchakavu wa
miundombinu ya maji hasa miradi wa Ilula na Isimani.
v.
Kuchelewa
kupata fedha za matumizi mengineyo au kutengewa kiasi kidogo cha fedhakisicholingana
na mahitaji halisi.
vi.
Kupanda kwa
gharama za umeme wa kuendeshea mitambo ya kusukuma maji katika mji wa Mafinga
na mamlaka ya maji ya IRUWASA
vii.
Uchache wa
fedha kwa ajili ya ujenzi, ukarabati na upanuzi mkubwa wa miradi ya zamani kama
miradi ya Mbalamaziwa na Malangali, Isimani na Ilula
9.0 Mikakati ya Mkoa ya Kukabiliana na Changamoto Zilizopo
i.
Kuandaa mpango
wa uvunaji wa maji ya mvua na kuatafua fedha kwa ajili ya utekelezaji wake.
ii.
Idara za maji
za kila Halmashauri zinaendelea kutoa elimu kwa Wananchi kuhusu uundaji na
Usajiri wa Jumuiya za watumiamaji, ufunguaji wa mifuko ya maji uendeshaji na
utunzaji wa miradi ya maji mijini na vijijini kwa mujibu wa sheria ya maji Na.
11 na 12 ya mwaka 2009 na Sera ya maji ya mwaka 2002.
Mwisho
Ndugu
Mgeni Rasmi
Tunayo furaha kubwa kukubali mwaliko wetu na
kushiriki kwako katika uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya maji Kimkoa
yanayofanyika leo tarehe 17 Machi, 2014 katika kijiji cha Ilamba, Halmahsuri ya
wilaya ya Kilolo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni