Jumamosi, 26 Aprili 2014


MATUKIO KATIKA PICHA MIAKA 50 YA MUUNGANO NGAZI YA MKOA WA IRINGA

Mamia ya wananchi wa Kijiji cha Kisanga na maeneo ya jirani waliojitokeza katika maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano ngazi ya Mkoa wa Iringa

Baadhi ya mamia ya wananchi wa Kijiji cha Kisanga na maeneo ya jirani waliojitokeza katika maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano ngazi ya Mkoa wa Iringa

 Wakuu wa Idara na mashirika mbalimbali waliohudhuria maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanzania ngazi ya Mkoa yaliyofanyika wilayani Mufindi
 Kwaya ya KKKT Kisanga ilitumbuiza 

 Kwaya ya Wanafunzi wa shule ya Msingi Kisanga wakiimba wimbo wa miaka 50 ya Muungano

 Wanafunzi wa shule ya msingi Kisanga akipiga mgoma

 Kwaya ya Nzivi ikitumbuiza

 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, Paul Ntinika akipangua Mashairi kuhusu umuhimu wa miaka 50 ya Muungano

 Kwaya ya KKKT- Kisanga ilitumbuiza

 Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Iringa ambaye pia ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Scolastica Mlawi akisoma Hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa

 Scolastica Mlawi akisisitiza jambo katika maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano

 Pongezi baada ya Hotuba nzuri

Mheshimiwa Diwani akitoa shukrani baada ya maadhimisho

MIAKA 50 YA MUUNGANO IMELETA MAFANIKIO NCHINI



Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Mkuu wa Mkoa wa Iringa amesema kuwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umeleta mafanikio makubwa katika nyanja zote nchini.
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Iringa ambaye ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa, Bibi. Scolastica Mlawi (katikati) akifuatilia burudani mbalimbali

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Scolastica Mlawi katika Maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika katika kijiji cha Kasanga, Kata ya Kasanga, Tarafa ya kasanga wilayani Mufindi.

Dkt. Ishengoma amesema “muungano umeleta manufaa makubwa katika nyanja za kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni, jukumu letu ni kuuenzi, kuudumisha na kuuimarisha kwa masilahi ya vizazi vya sasa na vijavyo”.  Amesema kuwa manufaa yatokanayo na Muungano huu ni pamoja na kudumishwa kwa amani, upendo, umoja, mshikamano na ushirikiano miongoni mwa jamii ya Tanzania Bara na Tanzania visiwani.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa amesema kuwa waasisi wa Muungano walikubaliana kushirikiana katika mambo mengi. Ameyataja baadhi ya mambo hayo kuwa ni katiba na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mambo ya nchi za nje, ulinzi na usalama, polisi, mamlaka juu ya mambo yanayohusika na hatari. Mambo mengine ni pamoja na uraia, uhamiaji, mikopo na biashara za nje, utumishi katika serikali ya Jamhuri ya Muungano na kodi inayolipwa na watu binafsi na mashirika. Ameyataja mambo mengine kuwa ni ushuri wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa nchini unaosimamiwa na idara ya forodha pamoja na ushirikiano wa bandari, usafiri wa anga na posta na simu.

Dkt. Ishengoma amewataka wananchi wote mkoani Iringa kuhakikisha wanaendeleza yale yote mambo mazuri yaliyoachwa na waasisi wa Muungano na kuyaboresha pale inapobidi. Aidha, amewataka wananchi wote kujitokeza na kushiriki katika shughuli za maendeleo ili kujiletea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.    

Maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanzania yameongozwa na kauli mbiu isemayo “Utanzania Wetu ni Muungano Wetu, Tuulinde, Tuuimarishe na Kuudumisha”.
=30=

MAZISHI YA DC CHANG'A YAFANYIKA IRINGA

MAZISHI

WIKI YA CHANJO MKOANI IRINGA

Na. Dajari Mgidange
Wazazi wametakiwa kuwapeleka watoto wao wenye umri chini ya miaka miwili kwenye vituo vya huduma za afya kupatiwa chanjo dhidi ya magonjwa mbalimbali.

Kaul;I hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma alipokuwa akizindua wiki ya chanjo katika mkoa wa Iringa uzinduzi uliofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Dkt. Christine amesema kuwa kumekuwa na ongezeko la watoto ambao hawajapata na wengine kutokamilisha chanjo zao matokeo yake kusababisha milipuko ya magonjwa ya mara kwa mara hasa ugonjwa wa surua. Amesema katika jitihada za kuzuia milipuko hiyo Tanzania inatarajia kutoa chanjo ya pili ya surua mwaka huu. Ametoa wito “kwa wazazi na walezi kuwapeleka watoto wote wenye umri chini ya miaka miwili ambao hawajapata chanjo au hawajakamilisha chanjo zao kwenye vituo vya huduma za afya wakiwa na kadi zao za kliniki lakini pia watoto ambao hawana kadi wapelekwe watapewa kadi na chanjo” alisisitiza Dkt. Ishengoma.

Amesema “kila mmoja wetu anawajibu wa kuhakikisha kuwa mtoto wake, mtoto wa jirani au mlengwa mwingine yeyote anapewa chanjo ili kuzuia asipatwe na maradhi ambayo yanakingwa na chanjo na asiwe hatari kwa wengine kwa kuwaletea ugonjwa”. Amesema kuwa chanjo ni jukumu la jamii nzima na hutolewa bila malipo yoyote na kuwahakikishia kuwa hazina madhara yoyote.

Mkuu wa Mkoa amesema kuwa wiki ya chanjo ni fursa ya kutoa ujumbe kuhusu chanjo mpya za kuzuia ugonjwa wa Nimonia na Kuhara kwa watoto na kuhamasisha jamii kufika vituoni ili kupata maelezo zaidi na huduma hiyo. Ujumbe wa wiki ya chanjo ni “Jamii iliyokamilisha chanjo ni jamii yenye Afya” ukiongozwa na kaulimbiu isemayo “Chanjo ni jukumu  letu sote”.

Amesema kuwa chanjo ni mkakati muafaka katika kutokomeza maradhi na kupunguza vifo vya watoto, hivyo kupunguza gharama kubwa kwa famila na Taifa kwa ujumla. Ameongeza kuwa chanjo huchangia kupunguza vifo vya watoto kati ya milioni mbili (2) hadi milioni tatu (3) Duniani kila mwaka yakiwemo maradhi ya Nimonia na Kuhara ambayo yamekua ni chanzo cha vifo vingi. Ameyataja magonjwa yanayokingwa hapa nchini na chanjo kuwa ni kifua kikuu, dondakoo, polio, surua, pepopunda, homa ya ini, homa ya uti wa mgongo, kichomi na kuhara.

Tanzania inaungana na nchi nyingine katika kuadhimisha wiki ya chanjo Duniani tarehe 24-30 April 2014. Katika mkoa wa Iringa ilizinduliwa katika kijiji cha Ulata Kata ya Wasa, Tarafa ya Kiponzelo katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.
=30=

Habari zinazoendelea hivi sasa

SERIKALI KUWEZESHA VIJANA KUKOPA

Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa Serikali itaendelea kuwawezesha vijana kwa kuwatengenezea mazingira mazuri ya mikopo ili waweze k...