Mshauri
wa Mgambo Mkoa wa Iringa ametakiwa kusimamia zoezi la medani la komaza 2016 ili
kuchochea kuwaandaa vizuri vijana kuwa wazalendo kwa nchi yao.
Agizo
hilo lilitolewa na mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza alipokuwa akifungua
zoezi la medani komaza 2016 lililofanyika Manispaa ya Iringa.
Masenza
alisema “askari hufanya mambo mengi
hususani misako na doria, kupambana na majambazi, kuzuia dawa za kulevya na
wahamiaji haramu na kuilinda nchi”. Aliongeza “juhudi hizo zinathibitisha kwamba jeshi la mgambo linaumuhimu mkubwa
kwa maendeleo ya Taifa letu, hivyo zoezi la medani komaza 2016 liwe kichocheo
kikubwa cha kuwaandaa vijana wetu kuwa askari wazuri, wazalendo, waadilifu,
watenda haki, jasiri na wenye dhamira ya uaskari”.
Aliwataka
wanamgambo hao kuhakikisha mafunzo watakayopewa yanatekelezwa kwa vitendo.
Aliongeza kuwa askari wanaoandaliwa wawe mfano wa kuigwa katika jamii
inayowazunguka. Alisema kuwa wanamgambo wengine wakipata mafunzo, huonesha
ubabe kwa jamii bila sababu ya msingi. “Sisi
tusifanye hivyo, mafunzo haya yatupe nidhamu ya kuwaheshimu wananchi
wanaotuzunguka na kuwasaidia” alisisitiza Masenza.
Mkuu
wa mkoa alipongeza juhudi za mshauri wa mgambo mkoa wa Iringa za kuwaandaa
vijana wanaoshiriki mafunzo ya mgambo kuwa wakakamavu kiaskari ambao wako
tayari kuilinda nchi yao na kupambana na uhalifu wa aina yoyote katika mkoa wa
Iringa na Taifa kwa ujumla.
=30=
Naomba namba ya simu ya ofisi ya mgambo iringa
JibuFuta0785789102 hii yangu
JibuFuta