Jumamosi, 29 Aprili 2017

NEMC YAZIPIGA FAINI TOMMY DIARIES FARM NA NDOTO FARM MILIONI 20



Na Mwandishi Maalum IRINGA
Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (NEMC) limeyatoza faini mashamba ya mifugo ya Tommy na Ndoto jumla ya shilingi milioni 20 kutokana na kukiuka Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004.

Faini hizo zilitangazwa na wakili wa serikali mkuu kutoka NEMC, Benard Kongola baada ya kikosi kazi namba tatu cha kunusuru ikolojia ya mto Ruaha mkuu kukagua hali ya uhifadhi wa mazingira katika mashamba ya mifugo ya Tommy na Ndoto yaliyopo wilayani Kilolo Mkoani Iringa jana.
Mwanasheria wa NEMC Benard Kongola (kulia) akipokea maelezo ya Athanas Mushi wa shamba la Tommy Diaries Farm

Baada ya kitamka faini hizo, wakili Kongola alisema kuwa Shamba la mifugo la Tommy limetozwa faini kutokana na kulima mahindi na migomba ndani ya mita 60 kutoka ukingo wa mto Ruaha mdogo. Alisema kuwa shamba la mifugo la Ndoto limetozwa faini kutokana na kufanya biashara bila kuwa na cheti ya tathmini ya hali ya mazingira kutoka NEMC. 

Wakili Kongola alisema kuwa faini hizo zinatakiwa kuwa zimelipwa ndani ya siku 14 toka tarehe ya faini hiyo. Aliongeza kuwa baada ya siku 14 NEMC wataenda kukagua utekelezaji wa agizo hilo.

Kikosi kazi hicho kikiwa katika ukaguzi wa hali ya uharibifu wa mazingira katika shamba la mifugo la Tommy kilibaini uharibifu wa mazingira ikiwa ni pamoja na kupandwa miti isiyo rafiki kwa mazingira na kusababisha kukauka kwa vyanzo vya maji.

Mwenyekiti wa kikosi kazi hicho ambaye pia ni Katibu Tawala mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu alisema “chanzo hiki cha maji ambacho kinaelekea kukauka lazima kihifadhiwe ili kirudie hali yake ya awali. Miti hii yote ambayo si rafiki kwa mazingira lazima ikatwe na kupandwa miti ambayo ni rafiki kwa maji na niletewe taarifa ya utekelezaji ndani ya wiki moja, alisema Ayubu”.

=30=

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Habari zinazoendelea hivi sasa

SERIKALI KUWEZESHA VIJANA KUKOPA

Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa Serikali itaendelea kuwawezesha vijana kwa kuwatengenezea mazingira mazuri ya mikopo ili waweze k...